![]() |
|
Ukosefu wa ajira ni changamoto kubwa
duniani kote. Hili linasikitisha kwa kuwa kazi ni chanzo cha heshima binafsi,
amani na utulivu.Tanzania, miongoni mwa nchi za dunia ya tatu,
imechukua hatua muhimu katika kuendeleza sekta yake ya ajira, japo bado
inakabiliwa na changamoto kubwa katika hilo.
Asilimia kubwa ya watanzania wenye
uwezo wa kufanya kazi, aidha hawana ajira au ajira walizonazo haziendani na
uwezo wao.
Kutokana na ushindani mkubwa katika
soko la ajira na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia kwenye soko la ajira
(800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka), sekta rasmi imekosa mafanikio katika
kuzalisha fursa za ajira, hasa mijini. Matokeo yake ni; kiwango cha
umasikini kimeongezeka.
Sababu kuu zinazochangia fursa duni
za ajira ni
pamoja na:-
· Kutokuwa
na usawa kati ya supply ya wafanyakazi na mahitaji. Ukweli ni kwamba, supply ya
wafanyakazi ni kubwa kuliko demand ya wafanyakazi katika soko la ajira. Kila
mwaka tunashuhudia ongezeko la vijana wanaomaliza masomo yao ambao wanaingia
mtaani kuongeza idadi ya watafutao kazi.
· Vijana
kukimbilia kutafuta kazi mijini. Asilimia kubwa ya vijana wakimaliza elimu yao,
hufikiria kwenda mijini kutafuta ajira, na wengi wao huwa na mawazo ya kufanya
kazi ‘za ofisini’.
Hili linasababisha shinikizo na ushindani mkubwa wa fursa za
ajira. Laiti kama vijana wengi wangeamua kujikita katika sekta ya kilimo cha
kisasa au sekta nyingine tofauti tofauti kwa kutumia elimu yao, ongezeko la
watafutao kazi mjini lingepungua kwa kiasi kikubwa.
· Elimu
duni. Hili linajumuisha kutokujua kusoma na kuandika na ukosefu wa mafunzo
sahihi yanayomuandaa mtu kuingia katika soko la ajira.
Hakuna mwajiri anayeweza
kuajiri mtu asiye na stadi muhimu za kitaaluma zinazohitajika katika kazi.
Inaaminika kuwa, zaidi ya 61% ya wahitimu wanakuwa hawako tayari kiushindani
katika soko la ajira.
Kutokana na mwangaza huo wa hali
halisi ya ajira nchini Tanzania mradi wa #RecruitMe umejipanga
kusaidia kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, vijana na wazee ili waweze kupata
ajira wanazotaka. Tunafahamu kwamba ukosefu wa kazi ni jambo linalotatiza wengi
na wengi kuhisi kuwa wamenyimwa haki yao kama binadamu ndani ya jamii
wanayoishi.
Kwa hiyo, #RecruitMe kwa
makusudi mazima imeamua kujitolea kuweka jukwaa ambalo kila mtu anaweza
kulitumia anapotafuta ajira sahihi na kupitia jukwaa hilo, mtu anaweza kugundua
fursa mpya zilizopo katika soko la ajira.
Zaidi ya hayo, waajiri wanaweza
kunufaika sana kutokana na jukwaa hili, kwa kuwa linatoa fursa kwao pia
kutafuta wafanyakazi wanaowahitaji.
Lengo kuu la mradi huu si kuwapa
watu ajira yeyote tu, la hasha, bali ni kuwapatia watu ajira zenye hadhi,
heshima na kufanya ndoto za mtu kuwa kweli.
#RecruitMe itakupatia
ajira inayokubalika kisheria, yenye mapato yanayoendana na kiwango cha kazi na
ujuzi wako.
Tunakuthibitishia ajira itakayojali haki zako kama mwanadamu na
mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kujali maslahi yako.
Ili kupata huduma zetu, tafadhali
tembelea tovuti yetu http://goo.gl/zPLquy ambapo utakuwa na uwezo
wa kuona fursa za ajira mbalimbali, pamoja na kujenga profile yako mwenyewe.
Huna haja tena ya kutokwa na jasho kutembea kutoka ofisi moja hadi nyingine tu
na kuishia kunyimwa nafasi. Pumzika, na tembelea tovuti yetu. Tunaweza
kukusaidia kupata kazi uitakayo.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, November 23, 2015
Je, umejaribu #RecruitMe unapotafuta ajira Tanzania?
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment