CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP 2015 – ETHIOPIA:-Kilimanjaro Stars na Ushindi mnono wa 4-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 22, 2015

CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP 2015 – ETHIOPIA:-Kilimanjaro Stars na Ushindi mnono wa 4-0.

Timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imepata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya taifa ya Somalia kwenye mchezo wa kwanza kati ya timu hizo mbili kwenye michuano ya CECAFA Challenge Cup 2015 inayoendelea Addis Ababa, nchini Ethiopia.

 Magoli ya Kili Stars yamefungwa na Elius Maguri pamoja na John Bocco ‘Adebayo’ ambao kila mmoja amefunga magoli mawili kwenye mchezo huo.

Bocco alianza kuifungia Kili Stars goli la kwanza dakika ya 12 kwa mkwaju wa penati, Elius Maguli akapachika bao la pili dakika ya 17 na 54 kisha Bocco akahitimisha ushindi wa magoli 4-0 kwa kufunga bao dakika ya 55.

Kili Stars inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’ ipo kundi A pamoja na timu za Ethiopia, Somalia na Rwanda. 

Kili Stars itakutana na Rwanda kwenye mchezo wake wa pili siku ya Jumanne,November 24,2015 huku ikiwa inahitaji ushindi ili kujihakikishia kusonga mbele moja kwa moja kwenye hatua inayofuata ya mashindano hayo

Ikumbukwe jana,November 21,2015 timu ya visiwani Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ ilipoteza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Burundi kwa bao 1-0. 

Michuano hiyo imeanza rasmi November 21 na inatarajiwa kumalizika December 6 mwaka huu. 

KUNDI A
KUNDI B
KUNDI C
Ethiopia
Rwanda
Tanzania
Somalia
Kenya
Uganda
Burundi
Zanzibar
Sudan
Malawi
South Sudan
Djibouti
 
RATIBA/MATOKEO.

**Saa: Mechi ya Kwanza Saa 10 na ya Pili Saa 12

Jumamosi Novemba 21,2015.

Burundi 1 – 0 Zanzibar 

Ethiopia 0 – 1 Rwanda

Jumapili Novemba 22,2015.

Somalia 0 – 4 Tanzania 

Kenya Vs Uganda

Jumatatu Novemba 23,2015.

S. Sudan v Djbouti

Sudan v Malawi

Jumanne Novemba 24,2015.

Zanzibar Vs Uganda

Rwanda Vs Tanzania

Jumatano Novemba 25,2015.

Kenya Vs Burundi

Somalia Vs Ethiopia

Malawi v Djibouti

S. Sudan v Sudan



Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad