|
Dr Alok
Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka
hospitali ya Apollo akiongea na waandish wa habari katika cliniki iliyoanza
tarehe 11 na kuendelea mpaka tarehe 13 katika hospitali ya hindumandal.
|
|
Bwana
Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo
na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad akiongea na waandishi wa
habari katika Klinik hiyo.
|
|
Shamila Idd mama wa mtoto Zulea mwenye tatizo
la uti wa mgongo akiongea na waandishi wa habari katika kliniki iliyoandaliwa
na Dr Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo
kutoka hospitali ya Apollo.
Na Mwandishi Wetu,
Tanzania
ni moja ya nchi ambazo ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu
kitendo kinachopelekea nchi kupoteza fedha nyingi kwa kuwapeleka wagonjwa wa
matatizo ya aina hiyo nje ya nchi kupata matibabu na ushauri.
Inakadiriwa
kuwa watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa fahamu
hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa matibabu.
Kutokana
na hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini daktari
bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye pia ni Mkuu wa
idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali hiyo DKT ALOK RANJAN ambaye atakuwa akitoa
huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za nyuma.
Nao
baadhi ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika hospitali
ya hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuhakikisha kwamba
inasaidia katika gharama za matibabu ya watu wanaosafiri nje ya nchi kufuata
matibabu ya magonjwa mbali mbali.
Wamezitaka
pia kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za kimataifa
badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
Katika
mkutano huo na waandishi wa habari ulofanyika tarehe 12 katika hospitali ya
hindumandali Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali za Apollo amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa
maisha ili kuepukana na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo.
Anasema
kuwa kwa watu wazima ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya
ukaaji ambao hudhuru uti wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari,
uzito wa kupitiliza na sababu nyinginezo.
Tanzania
kwa sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa sasa
ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|





No comments:
Post a Comment