KOMBE LA CHALLENGE 2015:- Bingwa mtetezi Kenya ashushiwa kipigo na Zanzibar Heroes cha 3 -1 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 27, 2015

KOMBE LA CHALLENGE 2015:- Bingwa mtetezi Kenya ashushiwa kipigo na Zanzibar Heroes cha 3 -1

Wachezaji-wa-Zanzibar-na-baadhi-ya-viongozi-wakimpongeza-Abdallah-Othman-katikati-aliyesujudu
Timu ya Zanzibar  imeweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge CUP 2015 kama mmoja wa washindi watatu bora, baada ya kuifunga Kenya mabao 3-1 jioni ya leo November 27,2015,nchini Ethiopia.

Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Suleiman Kassim ‘Selembe’ mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja, wakati bao la Kenya limefungwa na Jacob Keli.

Rwanda imeifunga 3-0 Somalia, mabao ya Jacques  Tuyisenge, Yussufu Habimana na Hegman Ngomirakiza, wakati Sudan Kusini imeifunga 2-0 Malawi, mabao ya James Joseph Saed na Bruno Martinez.

Sudan imeifunga Djibouti 4-0, huku gwiji wake, Athar El Tahir akipiga hat-trick ya kwanza ya mashindano na bao lingine likifungwa na Faris Abdalla Mamoun.
Michuano hiyo itaendelea kwa mechi mbili kesho, kati ya Uganda na Burundi na Tanzania Bara dhidi ya Ethiopia zikihitimisha hatua ya makundi kuelekea Robo Fainali.

MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA CHALLENGE 2015.

Leo; Novemba 27, 2015.

Rwanda 3 - 0 Somalia

Zanzibar 3 -1 Kenya

Sudan Kusini 2 - 0 Malawi

Djibouti 0 - 4 Sudan

Kesho; Novemba 28, 2015.

Uganda Vs Burundi 

Tanzania Vs Ethiopia

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad