SERIKALI HAINA PESA:-Zimechotwa na nani? Wizara ya Fedha imetoa majibu yako Hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 27, 2015

SERIKALI HAINA PESA:-Zimechotwa na nani? Wizara ya Fedha imetoa majibu yako Hapa.

Kama umewahi kukutana na taarifa mitandaoni, kwenye vyombo vya habari au kwingineko basi ninayo majibu yote kutoka Wizara ya Fedha kuhusu ishu ya ukata wa Fedha Serikalini Tanzania.

Hii ni nukuu ya Kamishna Bajeti wa Wizara ya Fedha akitoa majibu ya pesa zilikotumika >>> “Watu waliokuwa wanaandikisha kupiga Kura, gharama zake ndizo tulizopeleka Tume ya Uchaguzi… Kwa mara ya kwanza katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika mwaka huu Uchaguzi umefanywa na fedha za Watanzania.”

IMG_20151127_161155

Kuna ukweli kuhusu Serikali iliyotoka madarakani kumaliza pesa zote? Majibu haya hapa >>> “Upatikanaji wa fedha uko hivi; hela zinazokusanywa leo zinaingizwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali Benki Kuu. Haiwezekani mtu akakomba hela kwa sababu zile hela zinaingia kila siku na kutoka, haiwezekani mtu akombe hela mfuko Mkuu wa Serikali… Kama kuna mtu amekomba hela msingesikia kwamba watumishi wa Serikali wameshindwa kulipwa mshahara? Mngesikia maandamano… tungeweza kufanya uchaguzi wetu wenyewe? vyuo vikuu wangepata hela za mikopo?… JK hakukomba hela hazina.” >>> Kamishna John Cheyo.

Habari kwa hisani ya Millardayo





Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad