ABIRIA PAZA SAUTI-KATIKA PICHA:-Tazama Matukio mbalimbali siku ya uzinduzi wa Kampeni Leo November 27,2015 Stendi ya Ubungo Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 27, 2015

ABIRIA PAZA SAUTI-KATIKA PICHA:-Tazama Matukio mbalimbali siku ya uzinduzi wa Kampeni Leo November 27,2015 Stendi ya Ubungo Dar es Salaam.

Pichani ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga ,akipaza sauti kuwaelimisha na  kuwahamasisha abiria kupaza sauti, pembeni yake ni balozi Kimera Hemed wakati wa- SIKU YA UZINDUZI WA KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI-LEO November 27, 2015,-Standi kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

 Abiria PAZA SAUTI ni kampeni maalumu inayotarajiwa kuendeshwa na taasisi ya mabalozi wa Usalama barabarani, yaani Road Safety Ambassadors (RSA) Tanzania kwaajili ya kukuza uelewa na kuwahimiza watanzania kutambua haki na wajibu wao wawapo safarini kama abiria.

Kamanda Mohammed Mpinga akisalimiana na baadhi na mabalozi wa Usalama Barabarani UBT leo,November 27,2015.

Mwenyekiti wa Kamati ya Matukio ya RSA bwana Jackson Kalikumtima akitoa elimu kwa mwananchi ambapo Kampeni ya PAZA SAUTI inawalenga abiria hasa wa mabasi ya mikoani kwakuwa kwanza wao ndio wanachukua idadi kubwa ya watumiaji wa barabara hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya.BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI JUU YA KAMPENI HIYO YA PAZA SAUTI

Wananchi wakifuatilia matangazo ya kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad