![]() |
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hellen Bisimba akizungumza
katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi 2015.
ASASI za
Kiraia (AZAKI) za nchini Tanzania zimebuni Ilani ya Uchaguzi na kuizundua rasmi
mbele ya hadhara, katika hafla iliyofanyika jana September 06,2015 jijini Dar es Salaam, na
kuhudhuriwa na viongozi wa asasi, wanasiasa na waandishi wa habari.
Na:-
Pendo Omary …mwanahalisionline.
Ilani hiyo imekusudiwa kuwa dira na
mwongozo wa kuzingatiwa na kila mshiriki katika hatua za uchaguzi mkuu wa mwaka
huu ambapo Watanzania wanatarajiwa kupiga kura tarehe 25 Oktoba.
Wananchi,
wagombea, vyama vya siasa, serikali na taasisi zake zenye jukumu katika
kusimamia taratibu zikiwemo za ulinzi na usalama kufanikisha uchaguzi mkuu kwa
lengo la kusaidia tume za uchaguzi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Pia ilani
hiyo ni mwongozo kwa waomba ridhaa ya kuongoza ambao wanawajibu wa kuzingatia
masuala ya msingi ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni yenye tija na
maslahi mapana kwa umma kwa maendeleo ya taifa.
Ilani hiyo
imebeba vipaumbele vikuu vya kuzingatiwa na vyama katika kutambua wajibu wao
kulingana na mahitaji ya wananchi wanaoingia katika kutafuta uongozi wa nchi.
Vipaumbele
hivyo ni Katiba Mpya, sera ya uchumi wa kitaifa (Sera inayolenga kulikwamua
taifa kiuchumi kwa kujenga mazingira sawa ya kiuchumi kwa Watanzania wote bila
ya kuweka matabanaka ya walionacho na wasionacho); usimamizi wa rasilimali za
umma na ulinzi wa haki za binadamu, utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa ilani hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora Tanzania, Bahame Nyanduga amesema ilani inalenga kuelekeza
wananchi, wagombea, tume za uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama na vyama vya
siasa katika kutoa mchango wao kwenye usimamizi wa taratibu za kufanikisha
uchaguzi mkuu.
Usimamizi
huo unapaswa kuwa imara usioruhusu mwanya wa hatua hizo kutekelezwa kwa nguvu
ya rushwa, hongo, matumizi ya nguvu upande wa vyombo vya ulinzi na usalama na
rasilimali ya umma.
Onesmo
Olengurumwa, Mkurugezi Mtendaji wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania – Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDs) – amesema wazo la
kuweka wazi matakwa ya AZAKI juu ya Tanzania wanayoitaka katika mfumo wa ilani
ya uchaguzi ilitokana na mkutano wa watetezi wa haki za binadamu uliofanyika 24
Julai, mwaka huu.
Lengo likiwa
ni kutathmini nafasi ya AZAKI katika michakato ya upanuzi wa demokrasia ukiwemo
uchaguzi mkuu.
“Mkutano huo
uliazimia pamoja na mambo mengine, kuundwa kwa kikosi kazi kitakachoandaa
rasimu ya ilani hii kwa niaba ya AZAKI. Inaleta faraja kwamba, ndoto hii
imeweza kutimia na kuwezesha kukamilika kwa ilani hii,” amesema Olengurumwa.
Miongoni mwa
asasi zilizochangia kubuniwa kwa ilani hiyo ya AZAKI, ni Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Mwamvuli wa asasi
zisizo za kiserikali Zanzibar (ANGOZA), Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA).
Uzinduzi wa
ilani hiyo umefanyika wakati vyama vya siasa vimo katika kipindi cha kampeni
kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kura itapigwa Oktoba 25
mwaka huu.
Siku
hiyohiyo, Wazanzibari mbali na kuchagua viongozi hao, watakuwa na kura nyingine
ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.
|
Monday, September 07, 2015
UMOJA WETU:-AZAKI wazindua Ilani ya Uchaguzi 2015 Tanzania.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment