UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Kupiga kura dakika moja. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 07, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Kupiga kura dakika moja.


Ni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25,2015 ambapo Kila kituo kitakuwa na watu 450 watakaotumia saa tisa huku Watu 52,000 waliojiandikisha mara mbili nao kupiga kura......


Ikiwa zimebaki siku 47 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, imebainika kuwa kila mtu atatumia wastani wa dakika moja kupiga kura kuchagua diwani, mbunge na rais.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema kila kituo kitakuwa na watu 450 watakaopiga kura kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.

Hiyo ina maana kwamba, kuanzia saa 2.00 mpaka saa 10.00 jioni ni sawa na saa tisa, ambazo ni sawa na dakika 540. Kwa sababu kila kituo kitakuwa na watu 450, ina maana kuwa watu hao watatakiwa kupiga kura ndani ya dakika 540 ambazo ni sawa na dakika 1.2 kwa kila mtu.

Kwa mujibu wa NEC, muda huo wa saa 10.00 jioni ni wa kufunga vituo, lakini watu ambao watakuwa katika mistari mpaka wakati huo wataendelea kupiga kura mpaka watakapomalizika.

Watu watakaojitokeza kuanzia muda huo hawataruhusiwa kupiga kura. Kituo kimoja watu 450 Lubuva amefafanua kuwa wakati wa uandikishaji, vilitumika vituo 37, 848 lakini wakati wa upigaji kura vitaongezeka ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura kwa sababu tofauti na uandikishaji, upigaji kura ni kazi ya siku moja tu tena kwa saa zisizozidi tisa.

Alifafanua kuwa ongezeko la vituo hivyo linalenga kuwahudumia Watanzania wote 23,782,558 waliojiandikisha kushiriki uchaguzi wa mwaka huu, akibainisha kuwa kwa mkakati ulioandaliwa, kila kituo kitatakiwa kuhudumia wapigakura wasiozidi 450 kwa saa tisa za siku hiyo, zitakazotumika kuamua mustakabali wa uongozi wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo.ZAIDI TAARIFA HII BOFYA HAPA.


 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad