![]() |
|
Rais Kikwete
na mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi
wengine katika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Morogoro ,Jana September 06,2015,Jumapili wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea huyo wa urais
kwa tiketi ya chama hicho tawala .
Mmgombea
Urais Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John
Magufuli amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu(October
25,2015) ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji.
Dk.Magufuli
alitoa kauli hizo jana wakati anazungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya
Mkamba,Ruaha,Mikumi,Kilosa mjini pamoja na Morogoro mjini ikiwa ni sehemu ya
kuomba ridhaa ya kuomba kichaguliwa urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema kuwa
serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na hivyo atapunguza
bei ya saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa
hivyo."Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi
wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na
saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo lazima
tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.
Kwa upande
mwingine alisema atasimamia amani ya nchi kwani ndio msingi wa maendeleo ya
taifa letu na kuongeza shida ya watanzania si vyama vya siasa bali ni maendeleo
yao.Kwa
picha zaidi BOFYA HAPA
|
![]() |
|
Sehemu ya
gharika la wananchi katika Uwanja wa
Jamhuri Mjini Morogoro Jumapili kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kwa
tiketi ya chama hicho tawala cha CCM.
|
![]() |
| Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |









No comments:
Post a Comment