![]() | |
|
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, kwenye
moja ya mikutano yake,Pichani ulifanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja
Mjini, Sepremba 2, 2015. Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa jana September 06,2015, alizua sintofahamu baada ya kusema; “CCM oyee”, kauli iliyowafanya wananchi hao kukaa kimya na walipoona akicheka waliitikia “oyeee” huku nao wakicheka na kumshangilia. Ingawa ilitokana na ulimi kuteleza, yeye mwenyewe alisema alitamka neno CCM kama utani ili kubaini ni wananchi wangapi wanaokishabikia chama hicho kati ya waliojitokeza uwanjani hapo kumsikiliza wakati tayari amekwishaeleza jinsi chama hicho tawala kilivyoshindwa kuliletea taifa maendeleo. Msindai kama Lowassa Wakati Lowassa akieleza kwamba alisema hayo kwa utani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai aliyekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, alitoa mpya baada ya kukiombea kura chama chake hicho cha zamani badala ya Ukawa kwenye mkutano wa hadhara. Msindai alitoa mpya hiyo juzi September 05,2015 ,jioni wakati akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Manyoni Magharibi na Mashariki uliofanyika Manyoni mjini kwa tiketi ya Ukawa.MWANANCHI.. Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
Monday, September 07, 2015
KAMPENI ZA UKAWA 2015:-.....''Sintofahamu ya LOWASSA...''jana September 06,2015.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment