KAMPENI UKAWA 2015:-Lembeli aanika yaliyofichwa Operesheni Tokomeza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 06, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:-Lembeli aanika yaliyofichwa Operesheni Tokomeza.

Mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA.

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameishambulia serikali ya CCM na kueleza kwamba serikali hiyo haiwezi kuwapatia wananchi maendeleo kutokana na kuwa na mfumo mbovu wa kiutawala. 

    Mbali na hilo Lembeli alisema serikali ya CCM ndiyo serikali pekee yenye mfumo kandamizi, viongozi wake ni walaghai wakubwa na imekuwa na mfumo mchafu wa kulindana mafisadi kwa mafisadi huku wananchi wa kawaida wakiendelea kutaabika.

Lembeli ambaye awali alikuwa mbunge wa CCM jimbo la Kahama na baadaye kutimkia Chadema, alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chadema zilizofanyika katika viwanja vya Freeman Mbowe ambapo uwanja huo ulijengwa na mbunge anayemaliza muda wake na kutetea jimbo hilo Prof Kulikoyela Kahigi.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo alitonesha vidonda vya wafugaji wa jimbo hilo kwa kueleza kwamba serikali imekalia ripoti ya uchunguzi wa Tume iliyoundwa na bunge kwa ajili ya Operesheni tokomeza.SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA..''


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad