UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:- Wafahamu wagombea wanne walioidhinishwa na NEC kugombea Ubunge Jimbo la Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 21, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:- Wafahamu wagombea wanne walioidhinishwa na NEC kugombea Ubunge Jimbo la Ngara.

Mgombea wa CHADEMA / UKAWA Jimbo la Ngara mkoani Kagera Bw.Peter Simon Bujari akiwa nje ya ofisi ya Afisa uchaguzi Jimbo la Ngara/Halmashauri ya wilaya ya Ngara mara baada ya kurudisha Fomu za Kugombea Ubunge  Makao Makuu ya Ofisi za Tume hiyo.
Bw.Peter Simon Bujari kushoto akiwa sambamba na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ngara , Bw.Kenedy Stanford Festo  nje ya ofisi ya Afisa uchaguzi Jimbo la Ngara.
Mgombea wa ACT Wazalendo,Bw.Dotto Jasson Bahemu. 

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM,Bw.Alex Raphael Gashaza (mwenye shati la Kijani ) naye karudisha Fomu za Kugombea Ubunge  Makao Makuu ya Ofisi za Tume hiyo.
 
Jumla ya wagombea wanne wa Ubunge katika jimbo la Ngara Mkoani Kagera leo August 21, 2015 wamerudisha fomu za kugombea nyadhifa hiyo katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani humo.

Msimamizi wa uchaguzi wilayani Ngara Bw. Cornel Ngudungi amewataja wagombea hao kuwa ni Bw.Dotto Jasson Bahemu wa chama cha ACT wazalendo ( akihama kutoka CCM ), Bw.Peter Simon Bujari wa CHADEMA, Bw. Alex Raphael Gashaza wa CCM na Bi. Helen Adrian Ghozi wa NCCR- Mageuzi -( akihama kutoka CCM).

Bw. Ngundugi amesema kuwa katika kipindi cha kampeni zinzoanza kesho August 22,2015 wagombea wanatakiwa kufuata sheria na taratibu katika kunadi sera na irani za vyama vyao na kusema kuwa ofisi yake haitawavumilia wale watakaoenda kinyume na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC.

Kampeni za uchaguzi mkuu kwa wagombea wa ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani zinaanza hapo kesho August 22, 2015 nchi nzima baada ya leo August 21,2015 kuwa siku ya mwisho wa kurudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi nchini Tanznaia ambapo siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi hao October, 25 mwaka huu 2015.


PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.   
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad