Mgombea
Urais kutoka chama cha TLP, Macmillan Lyimo
alipofika Ofisi za Tume ya Uchaguzi- NEC.
|
Nao
wanasiasa wakongwe nchini, Christopher Mtikila na John Lifa- Chipaka wametupwa
nje ya kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kutokana na kushindwa kutimiza vigezo vya kisheria.
Mchungaji
Mtikila anawakilisha Chama cha Democratic Party (DP) na Chipaka anawakilisha
Tanzania Democratic Alliance (TADEA). ...Vyama vyote hivyo vilianzishwa mara tu
Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa, Na. 11 ya 1992, ilipopitishwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano.
Kupitia
sheria hiyo, ndiyo ilitolewa ruhusa ya kisheria ya kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. Kabla ya sheria hiyo, masuala ya siasa
yalikuwa si katika mambo ya Muungano.
Pigo la
kukosa kuteuliwa kugombea urais, pia lilimpata Dk. Godfrey Malisa Kahangwa
aliyewakilisha Chama cha Kijamii (CCK), chama kilichoanzishwa miaka michache
iliyopita, baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.
Akitangaza
matokeo ya maombi ya vyama hivyo vitatu jioni hii, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema ombi la Mchungaji Mtikila
limekataliwa kwa sababu ameshindwa kuwasilisha tamko la kiapo la Mahakama Kuu,
ingawa yeye aliapa lakini mgombea mwenza wake ambaye hakutajwa jina, hakufika
na hakuna kiapo chake.
Jaji Lubuva
ambaye alifikia ngazi ya jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, amesema Dk.
Kahangwa hakutimiza idadi ya watu wanaotakiwa katika udhamini na amekosa
mgombea mwenza kutoka upande wa Zanzibar.
Kwa
Lifa-Chipaka, ilielezwa kwamba hakutimiza vigezo kwa vile alishindwa
kuwasilisha orodha ya wadhamini kutoka Zanzibar. .....kisheria walitakiwa watu 200
wenye kadi za kupigia kura.
Wakati
Chipaka amekosa wadhamini Zanzibar, upande huohuo chama hicho kimesimamisha
mgombea urais, ambaye ni Juma Ali Khatibu, Naibu Katibu Mkuu.
Jaji Lubuva
alisema kwa wote walioshindwa kutimiza masharti, maana yake wamekosa kuteuliwa
kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kwa utaratibu ulioandaliwa, hakuna muda wa kuwasubiri
kukamilisha taratibu.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp
+255789925630.
|
No comments:
Post a Comment