OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU:- Yafahamu Matokeo ya Pato la Taifa kwa robo Mwaka ya kwanza 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 14, 2015

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU:- Yafahamu Matokeo ya Pato la Taifa kwa robo Mwaka ya kwanza 2015.

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo August 14,2015 Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 ambayo yameonyesha kuwa thamani ya Pato la imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014. Kushoto kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa Daniel Masolwa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke wakati akitangaza matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 ambayo yameonyesha kuwa thamani ya Pato la imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka ya kwanza yaani kuanzia mwezi Januari – Machi, 2015 yameonyesha kuwa thamani ya Pato la Taifa imekua na kufikia shilingi trilioni 21.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 18.6 ya robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2014.

 
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Morrice Oyuke amesema takwimu hizo zimetayarishwa kwa kuzingatia marekebisho ya Takwimu za Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007.
 
Oyuke amesema kuwa, Pato hili la Taifa limeongezeka kwa kasi ya asilimia 6.5 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2015 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 8.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2014.....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad