Baadhi ya
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar.Picha
na Michuzi Jr.
NA BAKARI
ISSA WA GLOBU YA JAMII.
Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali
kuwa Mgombea
wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe
Magufuli
amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa
NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na
haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.
Hatahivyo,Nape
amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi
kimeanza ziara ya kampeni mapema.
Amesema watu
walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama
hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti
13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa
kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu 2015 katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli
yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya
Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa
kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.
Kuhusu msimamo
wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema
wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya
kushindwa katika kura za maoni za chama.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp
+255789925630.
|
No comments:
Post a Comment