ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba amepotea kwenye uwanja wa siasa.
Hali hiyo imejitokeza leo August 09,2015 asubuhi wakati mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa alipotembelea Ofisi Kuu ya CUFBunguruni, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.
Katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu, Lowassa anawakilisha vyama
vinne vinavyounda UKAWA ambavyo ni Chadema yenyewe, CUF, NCCR-Mageuzi
pamoja na NLD.
Lowassa alifika kwenye ofisi za CUF saa 12.40 mchana lengo likiwa ni
kuzungumza na viongozi wa chama hicho akiwa ni mwakilishi wao kupitia
UKAWA.
Katika Safari hiyo walikuwepo pia wenyeviti wenza wa UKAWA -Freeman
Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Emanuel Makaidi (NLD).
Viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif; Naibu
Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya; Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu
Lissu; Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu na wabunge
wanaotoka vyama vinavyounda UKAWA.
Tofauti na ilivyotarajiwa kwamba, kujiuzulu kwa Prof. Lipumba
kungesababisha mpasuko ndani ya CUF, badala yake maelfu ya wanachama wa
CUF walifurika katika ofisi za chama hicho mapema leo kuanzia saa tatu
asubuhi.
Hakukuwa na vikundi vya watu katika majadiliano kuashiria kujadili
kuhusu kuondoka kwa Prof. Lipumba, badala yake nyimbo za kumsifu Lowassa
na Ukawa zilitawala.
Baada ya Lowassa kukaribishwa na mwenyeji wake Maalim Seif, alisema,
“…kwanza nawapa pole kwa Lipumba kuondoka,” kauli hiyo iliyopokelewa na
maelfu ya wanachama wa CUF waliofurika katika ofisi hizo kwa kusema
“Hatumtakiii…..Lipumba aende zake.”
Lowassa aliendelea “nilikuwa sijamaliza kusema. Nawapongeza kwa
uvumivu wenu na umoja wenu katika kipindi hiki baada ya kuondoka
Lipumba.
“Nimepata faraja sana kujiunga na Ukawa japo kumekuwa na misukosuko
ndani ya UKAWA. Ni lazima tuwe wamoja, mtunze kadi zenu za kupigia kura.
Mwaka huu lazima tushinde tena kwa kura asilimia 90 ili wakiiba
asilimia 10 tusisikie,” amesema Lowassa.
Hata hivyo Maalim Seif amesema, “tumepata faraja kubwa sana
kutembelewa na Lowassa. Hii ni kuthibitisha UKAWA bado tupo pamoja.
Hakuna kurudi nyuma, mbele kwa mbele mpaka Lowassa aingie Ikulu.
Zanzibar tupo tayari Maalim Seif ndiye rais. Tunasubili aapishwe.”
Kwa upande wake Duni amesema, wagombea wa UKAWA hawapo kwa nia ya
kusaka madaraka peke yake kama ambavyo inaelezwa bali kuhakikisha CCM
inaondoka madarakani na kila Mtanzania anapata haki sawa katika
kunufaika na rasilimali za nchi yake.
“Kama mnavyojua, nilikuwa waziri serikalini. Juzi nimeamua kuachia
madaraka baada ya kushauriana na viongozi wangu wa CUF ili nijiunge na
Chadema kuhakikisha CCM inaondoka madarakani. Tayari nimeandika barua
kwa rais ya kuachia madaraka. Na juzi tu nimetoka kumuaga rasmi,”
amesema Duni huku akishangiliwa na umati.
Hata hivyo, katika mkutano huo Mbowe amewaambiwa wananchi na wafuasi
wa UKAWA kuwa, “hii safari ya mabadiliko tumeipigania kwa miaka 25. Wapo
waliopoteza maisha, kuachika, kufilisiwa, vilema na wenye kesi katika
safari hii. Imekuwa ngumu. Akitoka kiongozi kati yetu akaona malengo
yetu hayaendani nae. Huyo hatufai.
“Leo tuna wagombea waliojiunga na Chadema hivi karibuni na wanagombea
urais na umakamu. Chadema hatugombei vyeo. Tupo tayari kufanya kazi na
wenzetu bila kujali wamejiunga lini na chama.”
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kwenye mkutano huo amewatoa
hofu wananchi kuhusu uvumi unaoenezwa kwenye mitandao kwamba “mgombea
urais na mgombea mwenza wake ni lazima wawe wanachama kupitia vyama
wanavyogombea kwa muda wa miezi mitatu.”
“Katiba zote mbili za Tanzania na Zanzibar ninazo hapa. Hakuna Katiba
wala Sheria inayosema mgombea wa urais na makamo wake ni lazima
watimize muda wa miezi mitatu tangu kujiunga na chama wanachokiwakilisha
katika uchaguzi huu. Huu ni uzushi.”
Lissu amesema, masharti yanayotolewa na katiba hizo ni kwamba,
mgombea wa urais na makamu wake ni lazima wateuliwe na chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungua
Wanachama na Wafuasi wa Vyama UKAWA waliofurika kwenye Makao Makuu ya
CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana
na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha
Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao
Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam
leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha
Wananchi CUF.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais
wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel
Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF,
Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano
wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na
Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim
Seif Sharif Hamad akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama
vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF,
Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika
Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe
akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA,
nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar
es salaam
leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama
cha
Wananchi CUF.
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR - Mageuzi,Mh. James Mbatia akiwahutumbia maelfu ya
wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA,
nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar
es salaam
leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama
cha
Wananchi CUF.
Mgombea
Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA,
nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar
es salaam
leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama
cha
Wananchi CUF.
Mwanasheria
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu
akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA,
nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar
es salaam
leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama
cha
Wananchi CUF.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutumbia
maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA,
nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar
es salaam
leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama
cha
Wananchi CUF.
Mwenyekiti
wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akimpongeza Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kuhutubia.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
No comments:
Post a Comment