Kikao cha
Baraza Kuu kilijadili nafasi ya mwenyekiti iliyoachwa na Profesa Lipumba na
suala hilo liliachiwa Mkutano Mkuu wa chama ambao utaitishwa baada ya miezi
sita kwa kuwa ndio wenye uwezo wa kufanya uchaguzi huo kwa mujibu wa katiba ya
CUF.
Akitoa taarifa
ya kikao hicho, Maalim Seif alisema Baraza Kuu limeunda kamati maalum ya watu
watatu itakayofanya kazi na katibu mkuu kwa miezi sita kabla ya Mkutano Mkuu
kukaa na kumchagua mwenyekiti na makamu wake, nafasi ambazo ziko wazi.
Waliochaguliwa
kwenye kamati hiyo ni Twaha Taslima ambaye ni mwenyekiti na wajumbe wawili
ambao ni Aboubakary Khamis Bakary (Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar) na
Sererina Mwijage (mbunge mstaafu wa viti maalumu).
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment