PICHA / AJALI:- Picha wakazi wachoma moto kituo cha polisi baada ya Mtoto Tabia Mkulukute akipoteza maisha kwa kugongwa na gari na kuzikwa leo Bunju ‘A’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 11, 2015

PICHA / AJALI:- Picha wakazi wachoma moto kituo cha polisi baada ya Mtoto Tabia Mkulukute akipoteza maisha kwa kugongwa na gari na kuzikwa leo Bunju ‘A’

Muonekano wa kituo cha Polisi  kilivyochomwa moto ,ambapo Wakazi wa Bunju ‘A’, wamechoma kituo cha polisi cha eneo hilo kwa kile kilichodaiwa kushindwa kuelewana na askari baada ya mwanafunzi wa darasa la nne kugongwa na gari na kufariki dunia.

 Tukio hilo lilitokea jana Julai 10,2015 saa tatu asubuhi gari aina ya Toyota Coaster lilipomgonga mwanafunzi huyo, Thabitha Omari (11) aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Bunju ‘A’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alifika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wakazi hao waliomweleza kuwa wanataka matuta yawekwe barabarani karibu na eneo la shule ili kupunguza mwendokasi wa madereva wa magari.

Walimweleza kuwa eneo hilo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

Hata hivyo, wakati Kamanda Wambura akifanya jitihada za kuzungumza na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Kinondoni, ili waje waweke matuta yaliyokuwa yakidaiwa, ghafla kundi la watu lilivamia kituo cha Polisi na kukichoma moto.

Akizungumzia kitendo hicho, Kamanda Wambura alisema: “Hatua kali za kisheria zitachukuliwa na tutahakikisha wahusika wanakamatwa kwakuwa wamesababisha hasara ya mali na nyaraka zilizokuwamo ndani na nje ya kituo.”

Nyaraka zilizoungua.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amewataka raia kuwa rafiki wa polisi badala ya kuwa maadui kwani wao ndiyo hulinda usalama wao na mali zao.

Baadhi ya Baiskeli zilizoungua.

Awali, baada ya mwanafunzi huyo kugongwa, wanafunzi walifunga barabara ya Dar es Salaam - Bagamoyo kwa muda wa saa kadhaa na kuamua kuandamana kuelekea kituo cha Polisi kabla hakijachomwa moto.



Ofisa Mtendaji Mtaa wa Bunju ‘B’ Abdillah Mkeyenge  akizungumza na wanahabari mkasa ulivyo tokea kama alivyoona.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kihonzile, Abdallah amelaani kitendo kilichotokea kwani hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya tukio la kugongwa kwa mwanafunzi na kuchomwa kituo moto, akisema labda kulikuwa na mambo mengine.



Omary Mbonde (katikati) ambaye ni mlezi wa mtoto Tabia Mkulukute, akizungumza na wana familia walipokuwa wakipanga taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho.Mtoto huyo alikuwa akisoma Darasa la 4A Shule ya Msingi Bunju ‘A’.

Baada ya kutokea ajali hiyo wananchi na wanafunzi walijawa na hasira na kufanya vurugu huku wengine wakilala barabarani na kuchoma kituo cha Polisi moto.Tabia Mkulukute aliyefariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo Bunju, Dar es Salaam.

Mama mlezi Zainabu Mkulukute katikati akiwa na waombolezaji wakimfariji


Mtoto Tabia ambaye aliyegongwa na gari Pichani mwenye gauni la njano, enzi ya uhai wake. (Picha na Khamisi Mussa).

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad