PICHA / AJALI :-Joshua Nassari apata ajali ya helikopita Arusha jana Julai 07,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 08, 2015

PICHA / AJALI :-Joshua Nassari apata ajali ya helikopita Arusha jana Julai 07,2015.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amenusurika kifo baada ya ndege aina ya helikopita aliyokuwa amepanda kudondoka akiwa katika ziara katika jimbo lake lilipo mkoani Arusha. .

 Nassari akiwa na abiria wengine ambao majina yao mpaka sasa hayajapatikana wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani, Arusha.
Afisa Habari wa  Chadema, Tumaini Makene amelithibitishia kutokea kwa ajali hiyo, huku akiahidi kutoa taarifa kamili muda mfupi ujao.

Kwenye ukurasa wa Twitter wa CHADEMA zimewekwa post kwamba Mbunge Joshua Nassari ndiye aliyepata ajali hiyo ya Helicopter, amepelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu pamoja na rubani na watu wengine ambao hawajatajwa, ni baada ya kunusurika.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad