PICHA 18 ZA AJALI NGARA:-Lori laanguka na kuharibika vibaya eneo la Kasharazi ,wilaya ya Ngara mkoani Kagera huku Wananchi wakiacha kutoa msaada na kuiba Mifuko ya Chumvi . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 07, 2015

PICHA 18 ZA AJALI NGARA:-Lori laanguka na kuharibika vibaya eneo la Kasharazi ,wilaya ya Ngara mkoani Kagera huku Wananchi wakiacha kutoa msaada na kuiba Mifuko ya Chumvi .

Ajali hii imetokea leo Julai 07,2015,majira ya jioni  saa 12,katika mteremko wa K9,barabara ya Ngara - Burundi eneo la Kasharazi ukilihusisha Lori la Mizigo,Likiwa limebeba Viroba vya Chumvi ambalo kutokana kuharibika vibaya halikufahamika haraka ni la kampuni gani wala namba zake za usajili.

Mashuhuda wamesema kuwa huenda chanzo cha ajali kikawa ni mfumo wa breki kujamu maana wakati linashuka mteremko huo taili zake zilikuwa zikiburuza kwa kutoa moshi na kunuka.

Katika Lori hilo kulikuwa na watu wawili Dereva na Tingo wake ambapo Tingo ametoka akiwa kajeruhiwa na kuwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi huku mpaka Makonda Blog inatoka eneo la tukio saa Moja usiku Dereva alikuwa hajatolewa kutokana na kubanwa na kebini ya Lori maeneo ya miguu huku akiwa hai na jitihada za baadhi ya Wananchi wakiendelea kumnasua kwa kutumia vifaa duni vya kukatia .




Huu ndio Muonekano wa Lori hilo lilivyoharibika Vibaya baada ya Ajali.



Picha juu na chini ni  baadhi ya wananchi wa kasharazi na wasafiri wengine wakiangalia namna ya kumnasua Dereva aliyekwama  kutokana na kubanwa na kebini ya Lori hilo ,akibanwa maeneo ya miguu yake huku akiwa hai.
Hapa tukivuta Kebini ya Lori ili kumnasua Dereva aliyekwama kutokana na kubanwa maeneo ya miguuni huku akiwa hai.

Hapa baadhi ya wananchi wa kasharazi na wasafiri wengine wakivuta kebini ya Lori kwa kamba ili kumnasua Dereva aliyekwama kutokana na kubanwa na kichwa hicho huku akiwa hai.




Pichani juu na chini ni baadhi ya wananchi wa kasharazi badala ya kutoa msaada wa kuokoa wao walikutwa na Makonda Blog wakiiba bila aibu mifuko ya Chumvi iliyomwagika kutoka katika Lori hilo na kutokomea majumbani mwao kama picha zinavyowaonesha walivyokosa uungwana.




Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad