RIDHAA URAIS CCM 2015:- Nape athibitisha tano bora ya Wagombea Urais wa CCM . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 11, 2015

RIDHAA URAIS CCM 2015:- Nape athibitisha tano bora ya Wagombea Urais wa CCM .


Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyoketi hadi usiku wa Kuamkia leo Julai 11,2015 imepitisha majina Matano ya Wagombea yaliyofikishwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ili kupata mgombea atakayewania Urais kupitia Chama hicho.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Bw Nape Nnauye amewataja walioidhinishwa kuwa ni Dr Asha Rose Migiro, Dr John Magufuli, January Makamba, Bi Amina Salum Ali na Bw Benard Membe.
Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa malalamiko yake mbele ya vyombo vya habari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha CC. Kulia kwake ni Adam Kimbisa.

Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinaamua na kutoa majina matatu yanayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu ili kupatikana jina moja la Mgombea Urais kupitia CCM

Hata hivyo katika baadhi ya wajumbe ambao ni Dr Emmanuel Nchimbi, Bi Sofia Simba na Bw Adam Kimbisa walisusia mkutano huo na kuondoka wakidai kutoridhishwa na maamuzi hayo ambapo Bw Nape amesema katika Demokrasia walio wengi ndio huwa washindi na kwamba wasioridhika wanaruhusiwa kukata rufaa.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad