USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE:-Tafadhali…..Abiria Kataa hii ya Kupakiwa kama Mzigo ndani ya Probox au Hiace. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2015

USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE:-Tafadhali…..Abiria Kataa hii ya Kupakiwa kama Mzigo ndani ya Probox au Hiace.

Ujazaji huu wa abiria katika magari haya Abiria tuukatae sasa kwa kila mmoja wetu atimize wajibu wake, ajali zitakoma au Vitendo vya uvunjifu sheria za usalama barabara zitapungua hapa nchini Tanzania.



 Ni Toyota Hiace namba T 565 CRR juu na gari godo aina ya Toyota Probox Namba T 562 CXT na T 629 CYR yalikutwa na RSA wakati yanafanya safari kati ya Biharamulo mkoani Kagera ,Bwanga hadi Buselesele mkoani Geita,yakikiuka sheria kwa uvunjifu wa sheria barabarani,kwa kosa la kupakia abiria zaidi . Picha zote kwa hisani ya ROAD SAFETY AMBASSADORS(RSA)-TANZANIA


Safari bado ndefu sana…tambua kuwa USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE …Anza sasa kuzuia ajali na uvunjifu wa sheria barabarani kwa Kutoa taarifa kwa Askari wa USALAMA BARABARINI ILI HATUA ZICHUKULIWE KWA WAKIUKAJI.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad