Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akisalimia maelfu ya
wananchi vijana waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, hivi majuzi
kwenye uzinduzi wa Mashindano ya 37 ya Michezo ya Shule za Sekondari nchini Tanzania
- UMISETA.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda pamoja na mambo mengine ,aligusia “Michezo inahitajika sana
katika jamii yetu.. Serikali lazima tuendelee kuhamasisha jamii itambue umuhimu
wa Michezo.
Maeneo mengi
unakuta kuna migogoro ya maeneo ya Shule kuchukuliwa na watu katika miji yetu,
huu ni udhaifu kwa idara ya mipango miji hakuna sababu ya hili kutokea.
Wakuu wa
Mikoa muhakikishe kila Shule na maeneo yake yanapimwa na yapewe hati ili
kulinda kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali, tusipofanya hivyo migogoro
ya ardhi haitapungua hata kidogo“– Waziri Mkuu Pinda. |
No comments:
Post a Comment