Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2018

Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama.

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo Jana Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

BOFYA HAPA CHINI KUYATAZAMA MATOKEO YOTE.
 

Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad