|
Meneja mradi
wa kampuni ya Kabanga Nickel wilayani Ngara mkoani Kagera Bw.Ray Kohlsmith ( kushoto ) akikabidhi dawa za malaria na vifaa tiba kwa uongozi wa wilaya ya Ngara katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo vikiwa
na thamani ya Sh 16.7 milioni....Picha na Shaaban Ndyamukama.
|
Kampuni ya
Kabanga Nickel inayofanya utafiti wa madini wilayani Ngara mkoani Kagera imetoa
dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya
Sh.16.7 milioni kwa idara ya Afya
wilayani humo katika mapambano dhidi ya
ugonjwa wa malaria.
Afisa tawala
wa Kampuni hiyo ,Bw.Endrew Msolo amekabidhi dawa hizo pamoja na vifaa
tiba kwa uongozi wa idara ya Afya
katika hafla fupi iliyofanyika
kwenye Zahanati ya kijiji cha
Bugarama wilayani Ngara.
Bw.Msolo
amesema dawa na vifaa tiba vilivyotolewa
vitatumika katika vituo vinne vya afya ambavyo ni Bugarama, Mumilamila,
Muganza na Mkubu ambapo kampuni hiyo itaendelea
kuisaidia jamii katika elimu afya na mazingira
“Tumekuwa
tukitoa elimu kwa jamii inayozunguka eneo la mradi kupambana na maralia mbapo
baadhi ya kaya zimepatiwa vyandarua na kuhimizwa kutunza na kuhifadhi
mazingira”Alisema Msolo.
|
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngara, Dr John Endrew ( aliyeshika kit ya dawa kulia ) amesema kuwa dawa hizo
zitasaidia kupunguza uhaba wa dawa ambao umekuwa ukijitokeza katika vituo vya
kutolea huduma za Afya wilayani humo
Dr Andrew
amewataka wakazi wa Ngara kufika katika
vituo cha afya pindi watakapohisi kuwa na dalili za malaria ili kupata matibabu
yanayostahili kuliko kuhudhuria Hospitali baada ya kuzidiwa na kuongeza gharama
za kutibiwa.
Aidha
Mwenyekiti wa kijiji cha Bugarama ,Jafari Said amesema Kampuni hiyo imekuwa
ikisaidia wananchi katika kuwapunguzia changamoto mbalimbali kwa lengo la
kuhamasisha upatikanaji wa maendeleo bila kujali tofauti za mazingira
“Katika
tarafa yetu ya Rulenge Kampuni hii imesaidia madawati na vitabu kwa shule za
msingi na sekondari na kutoa elimu ya afya kila kaya vikiwemo vikundi vya
kilimo na ufugaji”Alisema Said
|
|
Pamoja na
hayo Afisa tawala wilayani Ngara,Bw. Davidi Mafipa ( pichani kulia ) kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Ngara Costantine Kanyasu amesema Kampuni hiyo imechangia ujenzi wa maabara
katika shule za sekondari katika kusaidiana na wananchi.
Amesema
mwezi Aprili mwaka huu kampuni hiyo ilichangia ujenzi wa maabara kwa kutoa
vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 24 milioni katika shule ya sekondari
ya Keza na Bukiriro na kuisaida jamii katika maabara za shule hizo.
|
|
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
No comments:
Post a Comment