Waziri Mkuu
wa Mstaafu wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa amepokelewa na maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye
viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015.
Mh. Lowassa amepata
udhamini wa wana CCM 9,516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya
kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya
Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. |
No comments:
Post a Comment