MBIO ZA URAIS TANZANIA:-Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akichukua fomu mkoani Dodoma leo June 12, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 12, 2015

MBIO ZA URAIS TANZANIA:-Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akichukua fomu mkoani Dodoma leo June 12, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akichukua fomu za urais mkoani Dodoma leo June 12,2015.

 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda leo June 12,2015 amechukua fomu ya kuwania kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Pinda amechukua fomu hiyo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo mkoani Dodoma ambapo pia alipata fursa ya kuongea na wanahabari.

Katika mkutano wake na wanahabari amekataa kuelekezea mengi kama walivyofanya watangaza nia wenzake ili kutoingilia ilani ya chama chake.

Asema ana uzoefu wa uongozi na mafanikio yote ya wizara nchini yeye ndiye kiranja wake.

Apanga kuongeza ukuaji wa uchumi wa pamoja ili kuondoa umbali kati ya mwenye nacho na asiyekuwa nacho.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad