Timu mbili
za Majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania, Polisi na Ruvu Shooting zimeipa mkono
wa kwa heri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Msimu huu 2014/2015 .
Katika mechi za kufunga pazia la Ligi Kuu jana May 09, 2015, Ruvu Shooting ilifungwa
bao 1-0 na wenyeji Stand United mjini Shinyanga, hivyo kumaliza na pointi 29
sawa na Mgambo JKT na Prisons ambazo zimebebwa na wastani mzuri wa mabao.
Polisi imefungwa 1-0 na Mbeya City hivyo kumaliza na pointi 25, nayo inaungana
na Ruvu Shooting kuiaga Ligi Kuu na kuendeleza rekodi yake ya kupanda na
kuteremka msimu huo huo.
Ndanda FC imenusurika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga na kumaliza na
pointi 31.
Mechi nyingine za Ligi Kuu hapo jana, Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na
Prisons, Simba SC imeifunga mabao 2-1 JKT Ruvu, Coastal Union imepata ushindi
wa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar mabao 2-1 na Azam FC imetoka sare ya 0-0 na
Mgambo JKT.
Wakati Ruvu Shooting na Polisi zikiipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, tayari
Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga, Mwadui ya Shinyanga na Toto
Africans ya Mwanza zimepanda.
Msimu ujao 2015/2016, Ligi Kuu soka Tanzania bara unatarajiwa kuwa na timu
mbili zaidi, kutoka 14 hadi 16 ili kuiongezea ushindani na msisimko
zaidi.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment