Raia 60 wa Burundi wamesafirishwa kutoka Kituo cha Mapokezi cha Kasange wilayani Ngara mkoani Kagera na kupelekwa kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma kupewa hifadhi. |
Radio Kwizera
ikiwa Kambini Nyarugusu imeshuhudia Mabasi na Malori ya Shirika la Umoja wa
Mataifa linalowahudumia Wakimbizi, UNHCR yakiendelea kuwapeleka waomba hifadhi
hao Kambini humo wakitokea nchini Burundi.
Wakati huo
huo Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amewasilisha Nyaraka zake kwa Tume ya Uchaguzi
nchini humo, CENI ili kujiandaa na Kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi
June mwaka huu 2015.
Rais Nkurunziza
amewasilisha Nyaraka hizo hapo jana pamoja na Faranga Milioni 15 za Burundi kwa
Tume hiyo ya Uchaguzi na kuthibitisha rasmi kuwa atawania Muhula wa Tatu wa
Urais kwenye Uchaguzi ujao
Hayo
yanajiri wakati Maandamano na ghasia za kupinga asiwanie Muhula wa Tatu wa
Uongozi kwenye uchaguzi ujao vikiendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Mwandishi wa
Radio Kwizera Mjini Bujumbura nchini Burundi amesema Mandamano na ghasia
zinazoendelea nchini humo zimesababisha vifo vya Watu 15 hadi sasa.
Source:-Radio
Kwizera FM.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment