Baada ya mechi za
wikiendi iliyomalizika jana April 12, 2015, msimamo wa ligi kuu soka Tanzania
bara umebadilika isipokuwa kwa timu nne za juu.
Yanga SC wanaendelea kujikita zaidi kileleni baada ya jana kuongeza
pointi tatu wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City uwanja wa Taifa na
kufikisha pointi 46 katika mechi 21 walizoshuka dimbani.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC wenye pointi 38 kwa mechi 29
walizocheza.
Nafasi ya tatu wapo wekundu wa Msimbazi, Simba SC wenye pointi 35 baada
ya kucheza mechi 21.
Kagera Sugar wanaocheza leo dhidi ya Ruvu Shooting wanashika nafasi ya
nne kwa pointi 28 walizovuna katika mechi 21 walizocheza.
Mkiani kuna mabadiliko, Prisons waliotoka suluhu na Ndanda FC sasa
wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na pointi 21 sawa na wanaoburuza
mkia Polisi Morogoro lakini Wajelajela wana wastani mzuri wa magoli ya kufunga
na kufungwa.
Katikati kuna mabadiliko, baada ya Stand United kushinda jana sasa
wanashika nafasi ya sita (6) wakijikusanyia pointi 27 katika michezo 21
waliyocheza mpaka sasa.
Baada ya Mbeya City kufungwa jana sasa wameporomoka mpaka nafasi ya 9 wakiwa
na pointi 25 baada ya michezo 22.
Standings
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, April 13, 2015
VPL 2014/2015….angalia msimamo mpya baada ya mechi za Jana April 12, 2015.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment