Chama cha Mapnduzi
kimesema kipo tayari kuyaweka kapuni majina ya makada wake sita walioadhibiwa
kwa kosa la kuanza kapeni za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao
(2015)kabla ya muda.
Kimesema hatua
hiyo itakuja kama haitapokea ripoti ya kamati ndogo ya nidhamu inayoongozwa na
makamu Mwenyekiti wa chama hicho Philip Mangula kabla ya kumalizka kwa muda wa
uteuzi.
Tamko hilo la CCM
limetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika
mahojiano kuhusu hatma ya kifungo cha makada hao pamoja na msimamo wa chama
kuhusu makada wake wengine wanaodaiwa kutenda kosa kama hilo.
Nape alisema kwa
sasa kifungo cha makada hao hakifahamiki kitaisha lini na endapo watatupwa nje
ya mbio za kuwnaia urais wanapaswa kijilaumu wenyewe kwa makosa yao ya kukiuka
taratibu za chama.
Makada walio
katika kifungo ni pamoja na Waziri mkuu wa zaman Edward Lowassa,Waziri
wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe,Waziri
wa Kilimo,Chakula na Ushirika Stephen Wasira,Naibu Waziri wa
Mawasiliano na teknolojia January Makamba na Mbunge wa
Sengerema Willium Ngeleja.
Source:-Mtanzania.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment