PUMZIKENI KWA AMANI:-Taswira ya Mazishi ya pamoja kwa Abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Nganga Jana April 12, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 13, 2015

PUMZIKENI KWA AMANI:-Taswira ya Mazishi ya pamoja kwa Abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Nganga Jana April 12, 2015.

Mamia ya wakazi wa wilaya za kilosa na kilombero  wamejitokeza    katika mazishi  ya pamoja ya  watu kumi na tano kati ya kumi na tisa waliofariki katika ajali ya basi ya nganga ambalo liligongana na fuso jana April 12,2015 kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi  na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa mkoani Morogoro.

Wakizungumza kwa niaba ya serikali ,Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu waliofariki kwenye  ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari mkoani   Morogoro ili kudhibiti ajali za mara kwa mara zinazopoteza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na vilema  vya maisha   ambapo mkuu wa wilaya ya kilombero Bw Lephy Gembe amewataka  wananchi  kuwa na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.

Kwa upande wake Diwani  wa kata ya ruaha, Rahel Nyangasa amesema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi wa wilaya hizo huku ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo siwakusahaulika kwani umewastua sana ambapo naye  muinjilisti wa kanisa la kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na madereva wabovu.BOFYA HAPA KUTAZAMA PICHA ZA AJALI HIYO YA BASI NA FUSO.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad