|
Pichani kulia ni ndiye mganga wa jadi ambaye anatuhumiwa
kuwapa kinga Watuhumiwa wa kukata Mapanga na Koromeo ,Manispaa ya Bukoba ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Ibosa.
|
|
Hizi ni baadhi ya tunguli na madawa yaliyokuwa
yakitumiwa na wakata koromeo kama kinga.
|
|
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata
taarifa juu ya waliokamatwa kwa tuhuma ya kukata koromeo.
|
|
Afisa upelelezi wa mkoa wa Kagera Gilles
Muroto akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwaibambe.
|
|
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera,
Henry Mwaibambe akionyesha mazindiko yaliyokuwa yakitolewa na mganga wa jadi
aliyekamatwa na Jeshi hilo yaliyokuwa yakitumiwa na wakata Koromeo kama kinga.
|
|
Jeshi la polisi katika mkoa wa KAGERA limeanza
kufanikisha mikakati yake yenye lengo la kusambaratisha mtandao wa watu
wasiojulikana wanaojihusisha na vitendo vya kufadhili na kufanya mauaji ya
kuwakata kata watu kwa MAPANGA na baadae kuwanyonya damu ambavyo
katika kata za KITENDAGULO, KIBETA na RWAMISHENYE katika manispaa ya
BUKOBA.
Katika kusambatarisha mtandao huo jeshi
hilo limefanikiwa kuwaua watuhumiwa WAWILI, JOHANES JOSEPH
ambaye ni kinara wa mauaji ya kuwakata kata MAPANGA na EDWARD THEOPHIL
ambao ni miongoni mwa watuhumiwa WANNE walioshikiliwa kwa tuhuma ya
kuhusika na kufadhili vitendo mauaji ya kuwakata kata WATU kwa mapanga
kwa ajili ya imani za KISHIRIKINA.
Akizungumza April 09,2015 na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la
polisi mkoani KAGERA, HENRY MWAIBAMBE amesema watuhumiwa waliouwawa kwa kutumia
nguvu za giza walikuwa wakijaribu kuwatoroka maofisa wa jeshi la polisi
waliokuwa wakiwahoji wakati wakiwaonyesha MAZINDIKO wanayoyatumia
katika kutekeleza mauaji, pamoja na kutoa onyo kwa wanajihusisha na vitendo
hivyo pia amesema jeshi hilo kwamba linamshikilia GAUDENSIA
NDIBALEMA ambaye ni mganga wa jadi kwa tuhuma ya kuwapatia kinga wanajihusisha
na vitendo vya mauaji hayo.
Kufuatia vitendo vya mauaji ya kukata watu kwa
mapanga katika manispaa ya BUKOBA, zaidi ya watu KUMI wameishauwawa , vitendo
hivyo vinahusishwa na imani za kishirikina ambapo inadaiwa kwamba wale
wanaokatwa mapanga damu zao zinavyonywa na kupelekwa pasipojulikana.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|





No comments:
Post a Comment