EPL 2014 / 2015:-Taswira Picha wakati Arsenal wakiifunga Burnley 1 - 0 leo April 11,2015 na Sasa Pointi 4 tu dhidi ya Chelsea. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 11, 2015

EPL 2014 / 2015:-Taswira Picha wakati Arsenal wakiifunga Burnley 1 - 0 leo April 11,2015 na Sasa Pointi 4 tu dhidi ya Chelsea.

Aaron Ramsey akipongezwa na wachezaji wenzake wa Arsenal, Olivier Giroud (kushoto) na Hector Bellerin baada ya kufunga bao pekee leo April 11, 2015 kwa Timu ya Arsenal ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Burnley Uwanja wa Turf Moor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.


Shukrani kwake kiungo Aaron Ramsey, aliyeifungia bao hilo pekee The Gunners mapema dakika ya 12 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua. 


Ushindi huo wa nane mfululizo katika Ligi Kuu, unaifanya Gunners ipunguze idadi ya pointi inazozidiwa na vinara Chelsea hadi kubaki nne. 

Chelsea ina pointi 70, baada ya kucheza mechi 30, wakati Arsenal ina pointi 66 za mechi 32, ikifuatiwa na Manchester United pointi 62 mechi 31, ambayo kesho Jumapili April 12,2015  itamenyana na mahasimu Manchester City wenye pointi 61 mechi 31 pia. 

Burnley inazidi kutitia mkiani, sasa ikishika nafasi ya pili kutoka mkiani, kwa pointi zake 26 za mechi 32, mbele ya Leicester City pointi 25 mechi 31.  


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad