PICHA / AJALI:- Taswira ya Ajali mbili zilizotokeoa leo April 12, 2015 kwa Lori la mafuta kugongana na basi la abiria uso kwa uso na ile ya Fuso na basi kuwaka Moto na kuua watu 18. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 12, 2015

PICHA / AJALI:- Taswira ya Ajali mbili zilizotokeoa leo April 12, 2015 kwa Lori la mafuta kugongana na basi la abiria uso kwa uso na ile ya Fuso na basi kuwaka Moto na kuua watu 18.

Basi la Burudani likionekana mara baada ya ajali hiyo kutokea huko eneo la Soni, jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga. 


Abiria zaidi ya 50 wamenusurika Kifo leo April 12, 2015,baada ya basi walilokuwa wakisafiria liitwalo Burudani kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni mkoani Tanga. 

Mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokea baada ya Lori la mafuta kukatika breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. 

Habari zinasema hakuna maafa yaliyoripotiwa hadi sasa ila watu kadhaa wamepata majeraha na kukimbizwa hospitali.
Hii ni ajali ya pili ya basi la abiria kutokea leo April 12, 2015, ikufuatiwa na ile ya asubuhi Pichani juu na Chini,maeneo ya Msimba, Mikumi, jirani na milima ya Udzungwa ambapo imeripotiwa kwamba watu 18 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 10 kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na basi la abiria na yote mawili kushika moto hapo hapo.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad