Serikali ya
Tanzania imesema hakuna mtanzania aliyeuawa katika matukio ya mauji ya
chuki za kibaguzi (ZENOPHOBIA) yanayofanywa na raia wa Afrika Kusini
dhidi ya wageni na tayari imeanza mpango wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21
kati ya 23 waliohifadhiwa katika kambi kwenye mjini DURBUN nchni humo kwa ajili
ya usalama.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo April 20,2015,Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa Mhe. Bernad Membe (Pichani ) amesema vifo vya
watanzania watatu vilivyotokea nchni humo havina mahusiano na mauaji hayo
ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya afrika kusini imeanza kuchukua hatua na
tayari watu watatu waliohusika na kifo cha rais wa msumbiji wamekamatwa.
Akizungumzia
idadi ya watanzania waliohifadhiwa kwenye Kambi katika mji wa DURBUN,Mhe
Membe amesema takribani watanzania 23 wamehifadhiwa katika kambi ya isipingo
iliyo na zaidi ya raia wa kigeni elfu tatu ambao wako chini ya
ulinzi wa serikali ya afrika kusini na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa
kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati yao.
Akielezea
msimamo wa Tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA yanayoendelea nchni
afrika kusini,Mhe. Membe amesema serikali inaunga na jumuiya ya nchi za SADC
kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchni humo ambapo watu 8 wamekwisha
uawa kikatili na kuita serikali ya afrika kusini kuzuia mauaji hayo haraka
iwezekanavyo.
Aidha
amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la Watanzania kurudi nchni
humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande wa wafanyabishara walisajiliwa kihalali
na kupoteza mali zao, serikali itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna
ya kutafuta namna ya nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.
Amesema
tatizo hilo lilianza mwaka 2008 na 2014 na kwamba lilichangiwa na Mfalme Goodwill
Zwelithini wa Jamii ya Wazulu kuchochea fujo hizo dhidi wageni lakini Mfalme
huyo leo na amezungumza na wananchi hao akiwaasa kuacha kuwaua wageni waliopo
nchini humo
Waziri Membe
amewataja Watanzania waliofariki nchini Afrika Kusini kwa sababu ambazo ni
tofauti na vurugu hizo kuwa ni Bw Rashid Jumanne aliyeuawa baada ya kufanya
unyang'anyi, Athuman China aliyechomwa kisu akiwa gerezani kwa vurugu na Ally
Mohamed aliyekuwa na ugonjwa wa kifua kikuu na kwamba mwili wake umeletwa
nchini jana April 19, 2015.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
thanks for sharing
ReplyDelete