FA CUP Mei 30,2015:-.Rasmi Arsenal dhidi ya Aston Villa baada ya Liverpool kuzabwa 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 20, 2015

FA CUP Mei 30,2015:-.Rasmi Arsenal dhidi ya Aston Villa baada ya Liverpool kuzabwa 2-1.

Jana April 19, 2015,Aston Villa watakutana na Mabingwa Watetezi wa Kombe la FA, Arsenal kwenye Fainali ya FA CUP baada ya  kutoka nyuma na kuitandika Liverpool Bao 2-1 katika Mechi ya Nusu Fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembley Jijini London.

 Jumamosi April 18, 2015 , Arsenal, kwenye Nusu Fainali nyingine, walitumia Dakika 120 kuifunga Timu ya Daraja la chini Reading Bao 2-1 na kutinga Fainali.


Liverpool, wakiongozwa na Nahodha wao Steven Gerrard ambae kumbukumbu ya Siku yake ya Kuzaliwa ni Mei 30 Siku ya Fainali ya FA CUP kitu ambacho Liverpool walikiota kitatokea Gerrard kubeba Kombe, ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 30 la Philippe Coutinho aliepokea pasi ya Raheem Sterling lakini Dakika 6 baadae Straika wa Aston Villa Christian Benteke alisawazisha Bao hilo baada ya kuikamata pasi safi ya Fabian Delph.

Hadi Mapumziko Aston Villa 1 Liverpool 1

Kipindi cha Pili, Dakika ya 54, Fabian Delph alianzisha muvu safi na kumpa Benteke aliemsogezea Grealish aliemrudishia Fabian Delph na kupiga Bao la Pili safi na la ushindi.

Fainali ya FA CUP itachezwa Mei 30 Uwanja wa Wembley.

FAINALI

Jumamosi Mei 30,2015.

Arsenal v Aston Villa
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad