UEFA 2014/2015:-Licha ya Bayern Munich na FC Barcelona zafuzu Nusu Fainali ila kuchanika Suruali ya Pep Guardiola ni Habari ya Mjini. .Tazama Picha '' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 22, 2015

UEFA 2014/2015:-Licha ya Bayern Munich na FC Barcelona zafuzu Nusu Fainali ila kuchanika Suruali ya Pep Guardiola ni Habari ya Mjini. .Tazama Picha ''

Bayern Munich ilikaza na  kushinda kutoka kwenye  matokeo ya 3-1 ya wiki iliyopita na  kuendelea na matumaini kwenye michuano ya UEFA msimu huu 2014/2015 huku Kocha Pep Guardiola akifikisha mechi 100 jana April 21, 2015 akiwa anai-manage Bayern Munich, hivyo sherehe yake ilikuwa nzuri kiasi cha suruali yake kuchanika kama picha zikionesha.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani na FC Barcelona ya Hispania zimetinga Nusu Fainali katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao hapo jana April 21, 2015 usiku.

Baada ya kuchezea kichapo cha cha bao 3-1 katika mechi ya awali dhidi ya Porto FC ugenini,hatimaye Bayern Munic waliigeuzia kibao Porto na kuirarua bila huruma bao 6-1 na hivyo kuwa na njia nyeupe ya kutinga nusu Fainali kwa ushindi huo wa jumla ya magoli 7-4.
Nao FC Barcelona baada ya ushindi wa awali wa bao 3-1 dhidi ya Paris st Germen, mjini Paris ,hapo jana imeendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza bao 2-0,zilizowekwa kimiani na Mbrazil Neymar katika kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1.

Mechi nyingine za robo fainali zinakamilika hii leo April 22, 2015, pale Juventus ya Italia itakaposhuka dimbani kuwakabili Monaco ua Ufaransa,huku shughuli nyingine pevu ikitarajiwa kuonekana kwenye dimba la Santiago , pale mabingwa watetezi Real Madrid watakapo wakaribisha mahasimu wao Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad