LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Yanga SC hao na harufu ya Ubingwa bara baada ya kuichapa Mbeya City Uwanja wa Taifa April 12, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 13, 2015

LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Yanga SC hao na harufu ya Ubingwa bara baada ya kuichapa Mbeya City Uwanja wa Taifa April 12, 2015.

Kipa wa Mbeya City, Hanington Kalyesubula akiangalia mpira wavuni huku washabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao katika mechi ya Ligi kuu Vodacom Tanzania bara 2014/2015 hapo jana April 12, 2015  kwenye  Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kwa Vinara wa Ligi Kuu  Yanga SC  kuwatandika Mbeya City Bao 3-1 na kupaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 8 mbele ya Timu ya Pili Mabingwa Watetezi Azam FC.




Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwania mpira wa juu na beki wa Timu ya Mbeya City, Christian Sembuli wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo katika mchezo huo Bao za Yanga SC  zilifungwa na Mliberia Kpah Sean Sherman, Salum Telela na Kepteni Nadir Haroub 'Cannavaro'  na Bao la Mbeya City kufungwa na Themi Felix ambae hakumaliza Gemu baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Salum Telela.

Wachezaji wa timu ya Yanga wakisangilia ushindi ushindi na washabiki wao.Matokeo haya yamewabakisha Mbeya City Nafasi ya 8..Picha na Othman Michuzi.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad