|
Pichani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera
Bw.Vedastus Tibaijuka (Kushoto) na Afisa Elimu idara ya Sekondari wilaya
Bw.Julius Nestory wakiwa pamoja wakati Wadau
wa Elimu wilayani Ngara ,mkoani Kagera walipokutana hivi karibuni katika ukumbi
wa Shule ya sekondari Ngara mjini,pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu
ufaulu wa Kitaaluma na kupongezana baada ya shule kadha za Sekondari kutoa matokeo bora ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidaoto
cha nne mwaka jana 2014,wilayani humo.
Miongoni mwa
shule zilizofanya vizuri zaidi ni pamoja na Rulenge Sekondari,Rhec Sekondari,
Shule ya Sekondari ya Wasichana Baramba ambazo ni shule Binafsi wilayani humo pamoja
na Shule ya sekondari Kanazi ambayo ni ya Serikali na kuifanya wilaya ya Ngara
kushika nafasi ya 31 Kitaifa kati ya shule 16,693 za Sekondari nchini Tanzania.Habari/Picha na Shaban Ndyamukama.
|
No comments:
Post a Comment