MATUKIO MUHIMU:-Taswira Picha ya Utoaji wa Nishani za Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano April 26,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 27, 2015

MATUKIO MUHIMU:-Taswira Picha ya Utoaji wa Nishani za Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano April 26,2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana April 26,2015 viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dk.Mohammed gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam....TAZAMA PICHA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad