VPL 2014/2015:-Yanga SC Bingwa wa Tanzania bara 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 27, 2015

VPL 2014/2015:-Yanga SC Bingwa wa Tanzania bara 2015.

Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara msimu 2014/2015 ikiwa ni mara 25 baada ya kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo April 27,2015.

 Ushindi huu umewafikisha Pointi 55 huku wakibakisha Mechi 2 kumaliza Ligi na kufuatiwa na waliokuwa Mabingwa Azam FC ambao wana Pointi 45 na wamebakisha Mechi 3.

Shujaa wa Yanga SC hii Leo ni Straika kutoka Burundi Amisi Tambwe aliepiga Hetitriki na Bao 1 kufungwa na anaeongoza Ufungaji Bora kwenye Ligi Simon Msuva ambae sasa amefikisha Bao 17 akifuatiwa na Amisi Tambwe mwenye Bao 14.

Msimamo-Timu za Juu VPL 2014/2015.

1. Yanga SC Mechi 24 Pointi 55

2. Azam FC Mechi 23 Pointi 45

3. Simba SC Mechi 24 Pointi 41

4. Mbeya City Mechi 24 Pointi 31
Ushindi huu wa Yanga umepokewa kwa furaha, nderemo na vifijo toka Nchi nzima ya Tanzania huku Mashabiki wakishangilia Timu hiyo waliyoibatiza 'Timu ya Wananchi.' 

MABINGWA WA TANZANIA 

**Fahamu: Kuna wakati Ligi ya Bara na Visiwani Zanzibar ilikuwa moja

1965 : Sunderland (Dar es Salaam)
1966 : Sunderland (Dar es Salaam)
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam)
1968 : Young Africans (Dar es Salaam)
1969 : Young Africans (Dar es Salaam)
1970 : Young Africans (Dar es Salaam)
1971 : Young Africans (Dar es Salaam)
1972 : Young Africans (Dar es Salaam)
1973 : Simba (Dar es Salaam)
1974 : Young Africans (Dar es Salaam)
1975 : Mseto Sports (Dar es Salaam)
1976 : Simba (Dar es Salaam)
1977 : Simba (Dar es Salaam)
1978 : Simba (Dar es Salaam)
1979 : Simba (Dar es Salaam)
1980 : Simba (Dar es Salaam)
1981 : Young Africans (Dar es Salaam)
1982 : Pan African (Dar es Salaam)
1983 : Young Africans (Dar es Salaam)
1984 : KMKM (Zanzibar)
1985 : Maji Maji (Songea)
1986 : Maji Maji (Songea)
1987 : Young Africans (Dar es Salaam)
1988 : Coastal Union (Tanga)
1989 : Malindi (Zanzibar)
1990 : Pamba (Mwanza)
1991 : Young Africans (Dar es Salaam)
1992 : Malindi (Zanzibar)
1993 : Simba (Dar es Salaam)
1994 : Simba (Dar es Salaam)
1995 : Simba (Dar es Salaam)
1996 : Young Africans (Dar es Salaam)
1997 : Young Africans (Dar es Salaam)
1998 : Maji Maji (Songea)
1999 : Prisons (Mbeya)
2000 : Young Africans (Dar es Salaam)
2001 : Simba (Dar es Salaam)
2002 : Simba (Dar es Salaam)
2003 : Hamna Bingwa
2004 : Simba (Dar es Salaam)
2005 : Young Africans (Dar es Salaam)
2006 : Young Africans (Dar es Salaam)
2007 : Simba (Dar es Salaam) 
2007–08 : Young Africans (Dar es Salaam)
2008–09 : Young Africans (Dar es Salaam)
2009–10 : Simba (Dar es Salaam)
2010–11 : Young Africans (Dar es Salaam)
2011–12 : Simba (Dar es Salaam)
2012–13 : Young Africans (Dar es Salaam)
2013–14 : Azam (Dar es Salaam)
2014-15 : Young Africans

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad