ELIMU YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI:-Mbunge awezesha Bodaboda kutambua Sheria...Tazama Taswira Picha hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 29, 2015

ELIMU YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI:-Mbunge awezesha Bodaboda kutambua Sheria...Tazama Taswira Picha hapa.

Muonekano wa Pikipiki nje ya Nyumba ya Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera ambapo Waendesha Bodaboda wanapatiwa Mafunzo ya sheria za usalama barabarani yaliyoanza jana April 28, 2015 kwa  vijana 250 kutoka jimbo hilo la Muleba Kusini na yamefadhiliwa na  Mbunge wa Jimbo hilo  Profesa Anna Tibaijuka ambaye amesema vijana hao wahakikishe wanazingatia sheria.
Mkuu  wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera Bw Francis Isack akizungumza na Waendesha pikipiki maarufu bodaboda wilayani humo wakati wa mafunzo kwa waendesha Pikipiki hao na kuwataka kuepuka kubeba abiria zaidi ya mmoja na kuhakikisha wanavaa kofia maalum  na abiria wao ili kulinda  maisha yao bila kupata ajali kwa uzembe.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Muleba Inspector Fredrick Mpolo akitoa  mada ya  sheria  kwa waendesha pikipiki hapo Jana April 28,2015 ,amesema   matukio ya ajali yanachangiwa na kubeba abiria zaidi ya uwezo wa chombo au mwendo kasi pamoja na ulevi.

Bw Mpogolo amesema madereva hao wahakikishe wanakuwa na leseni katika kuendesha na vyombo vya moto  pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo kuwa na bima kuepukana na changamoto za  kuchukuliwa sheria na mamlaka husika.



Pia washiriki walishauri  askari wa usalama barabarani kuwa rafiki na bodaboda  na kuwasimamisha katika mazingira ambayo si ya hatari ili wasiwe chanzo cha matukio ya ajali...Picha na Shaban Ndyamukama. 
 
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad