EPL 2014/2015:- Manchester City wala kipigo chao cha 6 katika Mechi 8 na kumfanya Meneja wao Manuel Pellegrini kuwa tumbo joto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 13, 2015

EPL 2014/2015:- Manchester City wala kipigo chao cha 6 katika Mechi 8 na kumfanya Meneja wao Manuel Pellegrini kuwa tumbo joto.

Mchezaji Juan Mata  akimfunga bao Joe Hart dakika ya 67 na kuleta  furaha na starehe kubwa kwa Mashabiki wa Manchester United baada ya  timu yao  kuwabonda Jirani zao Manchester City Bao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza msimu huu 2014/2015 hapo jana April 12, 2015.

Ushindi huu wa Manchester  United umewaweka nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Timu ya 2 Arsenal na Pointi 4 mbele ya Manchester City ambao wako Nafasi ya 4.

Pia ushindi huu umemaliza uteja wa Manchester United wa kufungwa Mechi 4 mfululizo katika Dabi ya Manchester na kuhakikisha pia ile historia ya kutofungwa mara 5 mfululizo na Mpinzani yeyote inadumishwa.


MAGOLI.

Manchester  United 4

-Ashley Young, Dakika ya 14

-Marouane Fellaini 27

-Chris Smalling 73

Manchester  City 2

-Sergio Aguero, Dakika ya 8 na 89

Kipigo hiki kwa City kimeleta hali tete kabisa kwani ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 8 na hii itafanya Meneja wao Manuel Pellegrini kuwa tumbo joto.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad