|
Timu ya soka
ya Azam FC sasa inahitaji miujiza kutetea Ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania
bara msimu huu 2014/2015, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa
Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo April 11,
2015,kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Bao la Azam FC jioni ya leo limefungwa na kiungo Himid Mao Mkami, wakati la
Mtibwa limefungwa na mshambuliaji mkongwe, Mussa Hassan Mgosi.
Matokeo hayo sasa yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 38 baada ya kucheza mechi
20, sawa na vinara, Yanga SC wenye pointi 43.
Sare hii ya
pili mfululizo kwa Azam FC baada ya katikati ya wiki kutoka 1-1 pia na Mbeya
City, rasmi inaanza kuitamanisha Simba SC kuwania nafasi ya pili.
Simba SC ina pointi 35 baada ya kucheza mechi 21 na itakutana na Azam FC wiki
ijayo.
Kwenye mechi
nyingine Leo April 11,2015,Coastal Union imeshinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ikitoka
kufungwa mabao 8-0 na Yanga SC, Coastal leo ilikuwa timu tofauti Chamazi,
ikicheza soka maridadi na kupata ushindi muhimu wa ugenini.
Mabao ya Coastal yamefungwa na Rama Salim na Iker Obinna na sasa mabingwa hao
wa Ligi Kuu 1988 wanafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 23 na wanapanda
hadi nafasi ya sita kutoka ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Siku ya Jumapili zipo Mechi mbili na Vinara wa Ligi Yanga wako Nyumbani Uwanja
wa Taifa kucheza na Mbeya City ambayo iko Nafasi ya 7.
Jumapili
Aprili 12,2015.
Yanga SC v
Mbeya City
Stand United
v Polisi Moro
LIGI KUU
VODACOM MSIMAMO - 2014/2015.
1. Yanga SC
Mechi 20 Pointi 43
2. Azam FC
Mechi 20 Pointi 38
3. Simba
SC Mechi 21 Pointi 35
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment