HONGERA SANA:- Twiga Stars yafuzu kucheza michuano ya All African licha ya kufungwa 3-2 na She Polopolo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 10, 2015

HONGERA SANA:- Twiga Stars yafuzu kucheza michuano ya All African licha ya kufungwa 3-2 na She Polopolo.

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imefuzu kucheza michuano ya All African,baada ya leo April 10, 2015,Twiga Stars imefuzu licha ya kipigo cha mabao 3-2 lkutoka kwa Zambia, She Polopolo.


Ushindi wa mabao 4-2 ugenini Lusaka, Zambia ndiyo uliouikoa Twiga Stars kufuzu kwa jumla ya mabao 6-5.
 Katika mechi hiyo iliyopigwa Taifa, Twiga Stars waliongoza kwa mabao 2-0 ya Asha Rashid na Mwanahamisi Sherua.

Lakini kipindi cha pili kikawa kigumu iliporuhusu mabao matatu na kulala kwa 3-0.
Twiga sasa itakwenda Kongo- Brazzavile Septemba mwaka huu kwenye AAG.

Kikosi cha Twiga Stars kilikuwa; Fatuma Omar, Anastas Katunzi, Stumai Abdalla, fatuma Makusanya, Fatuma Isa, Sophia Mwasikili, Donisia Daniel, Amina Ally, Shelder Boniface, Asha Rashid na Mwanahamisi Shurua. 

Zambia; Hazel Natasha Nali, Rachel Nachula, Lweendo Chisamu, Joana Benai, Mary Mwakapila, Mary Wilomba, Misozi Chisa Rachel, Meya Banda, Annie Kibanjo, Grace Chanda na Barbra Banda.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad