LA LIGA 2014/2015:- Luis Suarez apiga bao huku Messi akifikisha bao la 400 kwa Barcelona ikishinda 2-0 leo April 18, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

LA LIGA 2014/2015:- Luis Suarez apiga bao huku Messi akifikisha bao la 400 kwa Barcelona ikishinda 2-0 leo April 18, 2015.

Lionel Messi (kushoto), Luis Suarez (katikati) na Neymar wakishangilia bao la Suarez dhidi ya Valencia leo April 18, 2015 na kuwafanya FC Barcelona kuendelea kuitumulia vumbi Real Madrid katika mbio za taji la La Liga 2014/2015, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Valencia Uwanja wa Camp Nou.

 Luis Suarez aliifungia Barcelona dakika ya kwanza, kabla ya Claudio Bravo kupangua penalti Nahodha wa Valencia, Dani Parejo dakika ya tisa. 

Lionel Messi akaihakikishia Barca pointi tatu dakika ya 90, ambalo linakuwa bao lake 400 tangu aanze kuichezea Barcelona.

Barcelona sasa inatimiza pointi 78 baada ya kucheza mechi 32, ikifuatiwa na Real Madrid yenye pointi 73 za mechi 31 huku Atletico Madrid wakishinda 2 - 1 dhidi ya Deportivo la Coruna  na kufikisha sasa Pointi 69 nafasi ya 3. Real Madrid inacheza usiku huu  na Malaga.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad