EPL 2014/2015:-Baada ya Chelsea leo April 18, 2015 kuishinda Manchester United 1-0 sasa Mechi 2 tu Kuwa Mabingwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

EPL 2014/2015:-Baada ya Chelsea leo April 18, 2015 kuishinda Manchester United 1-0 sasa Mechi 2 tu Kuwa Mabingwa.

Vinara wa Ligi kuu Uingereza msimu huu 2014/2015, Chelsea wameendelea kuongoza Ligi baada ya kupata ushindi wa bao 1 – 0 wakiwa Nyumbani Stamford Bridge , dhidi ya Manchester United na ikiwa watashinda Mechi zao 2 zinazofuata basi wao ni Mabingwa Msimu huu.

Ushindi huu umewapa Chelsea uongozi wa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Arsenal na Manchester United kubaki Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11 nyuma.

Chelsea walifunga Bao lao la ushindi Dakika ya 38 kupitia Eden Hazard baada ya pasi nzuri ya kisigino ya Oscar kwenye Mechi ambayo Manchester United walimiliki Mpira kwa Asilimia 70 dhidi ya 30 ya Chelsea.BOFYA HAPA UTAZAME MATUKIO PICHA ZAIDI


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad