LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC taabani kwa Mbeya City huku Azam FC akifuta Matokeo ya Sare leo Hii April 18,2015 mechi za Ligi kuu Tanzania Bara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC taabani kwa Mbeya City huku Azam FC akifuta Matokeo ya Sare leo Hii April 18,2015 mechi za Ligi kuu Tanzania Bara.

AZAM FC.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, AzamFC, Leo hii April 18, 2015 wakiwa  kwao Azam Complex, Chamazi, wamefuta balaa ya Sare zilizowaandama na kuichapa Kagera Sugar Bao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014/2015.

 Azam FC sasa wanatimiza pointi 42, baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya vinara, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21.

Mabao katika Mechi hiyo yalifungwa na  Frank Domayo kwa Azam FC katika Dakika ya 40 na Kagera Sugar kusawazisha Dakika ya 54 kwa Bao la Babu Ally lakini Gaudence Mwaikimba akaipa ushindi Azam FC kwa Bao lake la Dakika za lala salama.

Huko Morogoro, Polisi Moro waliichapa Ndanda FC Bao 2-0 kwa Bao za Edward Christopher, Dakika ya 64, na Said Bahanuzi, Dakika ya 74.
MBEYA CITY.

Huko Sokoine, Matumaini ya Simba SC kurudi kwenye michuano ya Afrika mwakani,  yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu na Matokeo hayo, yanaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22.

Wenyeji Mbeya City waliitwanga Simba SC kwa Bao za Paul Nonga katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza na la pili kufungwa na Peter Mwalyanzi katika Dakika ya 69.

Kesho Jumapili April 18, 2015 ipo Mechi moja tu ya Ligi huko Mabatini, Mlandizi kwa Wenyeji Ruvu Shooting watakapocheza na Mgambo JKT.

LIGI KUU VODACOM 2014/2015 - RATIBA

Jumapili Aprili 19,2015.

Ruvu Shooting v Mgambo JKT

LIGI KUU VODACOM MATOKEO.

Jumamosi Aprili 18,2015. 

Polisi Moro 2 – 0 Ndanda FC 

Mbeya City 2 – 0 Simba SC

Azam FC 2 – 1 Kagera Sugar

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad