............................
Wanahabari
wakimfuatilia Chikawe.
|
Waziri Chikawe
amesema hivi karibuni kumekuwa na matukio yanayotokana na baadhi ya viongozi wa
taasisi za dini kutoa matamko ambayo
yanaashiria kuingilia masuala ya kisiasa kinyume cha sheria ya vyama , sura ya
337 na kanuni zake pamoja na katiba zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
Alitoa mifano
ya viongozi wa taasisi za dini wanapokutana na kutoa matamko yanayolenga
kuwashawishi waumini wao wafuate maelekezo yao kuhusiana na masuala ya Katiba
Inayopendekezwa au kuhusu uchaguzi mkuu ujao, matamshi ambayo yanakiuka sheria
ya usajili wa taasisi hizo.
‘’Ni kweli
kuwa viongozi hao wa dini wana haki ya kushiriki katika masuala ya kisiasa kama
watu binafsi ila ni kinyume cha sheria
kutumia uongozi wao kuwashawishi waumini wao watekeleze matakwa yao ya
kisiasa,’’ alisema Chikawe.
Alisisitiza
kuwa serikali itachukua hatua kali kwa watu binafsi, vyama vya siasa na taasisi
za kidini zitakazobainika kuvuruga usalama na utulivu wa nchi, ikiwa ni pamoja
na kufuta usajili wa vyama vya kijamii na vya kidini ambavyo vitakiuka katiba
ya kuanzishwa kwao.
HABARI/PICHA
NA DENIS MTIMA/GPL
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi
na Michezo kila stori inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi
kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment